Enjoy the best quotes on Hekima , Explore, save & share top quotes on Hekima .
“Mungu hatakubali kuwa na mtu katika ufalme wake ambaye hatakubali kutawaliwa naye. Usikubali kutawaliwa na Ibilisi, kubali kutawaliwa na Mungu. Ni jukumu letu kuanza kuishi sasa kama vile tutakavyoishi mbinguni. Shetani anataka uwe na hekima ya duniani ili akupumbaze. Lakini hofu ya Mungu ndiyo msingi wa hekima ya kweli. Ukitaka asikupumbaze, pokea Roho ya Mungu kwa kubatizwa. Ukiipokea Roho ya Mungu utajua mambo ya Mungu, ambayo dunia haiwezi kujua.”
Enock Maregesi“Mfalme Sulemani alikuwa mtu mwenye hekima kuliko wote ulimwenguni. Anatushauri, “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa; Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na BWANA atakupa thawabu (Mithali 25:21-22). Yesu anasema jambo fulani linalofanana sana na hilo katika mafundisho Yake yaliyofuata (Mathayo 5:44-45). Kitendo cha kutukanwa, kupigwa, kushtakiwa au kulazimishwa kubeba mzigo mzito usio wa kwako kinaweza kusababisha mafutu mabaya kabisa katika asili ya binadamu. Yaani, chuki, hasira, ukatili na hata vurugu. Lakini pale wale waliobarikiwa kuwa na hekima wanapojikuta katika majaribu makubwa kama hayo tabia yao haitakiwi kuwa ya shari, inda au ya kulipiza kisasi. Bali inatakiwa kuwa ya kusaidia, kuwa na ridhaa ya kutenda mambo mema, na kuwa mwema kwa wengine siku zote.”
Enock Maregesi“Kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa raha ni rahisi kuliko kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa shida, na utahitaji imani kuendelea kumwamini wakati wa dhiki. Vipindi vigumu katika maisha yetu hutokea kwa kila mmoja wetu. Kuamini ya kwamba Mungu ana makusudi ya lazima kukuondolea vikwazo katika maisha yako ni vigumu sana wakati mwingine, lakini imani ndicho kitu cha muhimu zaidi unachotakiwa kuwa nacho katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa. Amani ya Mungu, ambayo huzidi hekima na maarifa yote ya kibinadamu, ni kuliamini neno la Mungu kwamba ni la kweli. Bila imani hutaweza kumfurahisha Mungu. Imani ni ufunguo wa nguvu, uwezo na neema ambavyo Mungu ametupangia. Kwa ufupi, Mungu ni mkubwa kuliko wewe na matatizo yako.”
Enock Maregesi