Yesu Quotes

Enjoy the best quotes on Yesu , Explore, save & share top quotes on Yesu .

Kilio kikuu cha Yesu, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?”, yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”, na “Imekwisha”, vilitabiriwa katika Zaburi 22 ili watu waliompinga Kristo waamini kama Yesu alikuwa Masihi. Zaburi 22 ulikuwa wimbo maarufu katika kipindi cha karne ya kwanza, kipindi ambacho Yesu alizaliwa na kufa, uliotungwa na mfalme Daudi, ulioitwa ‘zaburi ya mateso na matumaini ya mwadilifu’. Kwa hiyo Yesu aliposema maneno hayo yaliwaingia watu akilini, na kuanzia hapo imani hasa ya Ukristo ikachukua kasi hadi leo hii. Zaburi 22 inaanza na “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” na inaisha na “Imekwisha”, miongoni mwa maneno saba aliyoyasema Yesu pale msalabani Golgotha. Kwa hiyo, Zaburi 22 ni utabiri wa kifo cha Yesu.

Enock Maregesi
Save QuoteView Quote

Mfalme Sulemani alikuwa mtu mwenye hekima kuliko wote ulimwenguni. Anatushauri, “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa; Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na BWANA atakupa thawabu (Mithali 25:21-22). Yesu anasema jambo fulani linalofanana sana na hilo katika mafundisho Yake yaliyofuata (Mathayo 5:44-45). Kitendo cha kutukanwa, kupigwa, kushtakiwa au kulazimishwa kubeba mzigo mzito usio wa kwako kinaweza kusababisha mafutu mabaya kabisa katika asili ya binadamu. Yaani, chuki, hasira, ukatili na hata vurugu. Lakini pale wale waliobarikiwa kuwa na hekima wanapojikuta katika majaribu makubwa kama hayo tabia yao haitakiwi kuwa ya shari, inda au ya kulipiza kisasi. Bali inatakiwa kuwa ya kusaidia, kuwa na ridhaa ya kutenda mambo mema, na kuwa mwema kwa wengine siku zote.

Enock Maregesi
Save QuoteView Quote

Amri ya Kristo ilipima imani ya yule kipofu, ikiithibitisha na kuiimarisha. Bila kuchelewa au kusita, kipofu alitii amri ya Mungu: Alikwenda kuosha macho yake katika bwawa la Siloamu na aliona. Wengi wanaweza kuona ni kazi ya kipuuzi kwa mtu ambaye ni kipofu kufanya kazi ndogo kama hiyo ili aone. Lakini kwa vile alitii, kipofu alipona. Baraka huja kupitia utii. Kwa maana nyingine, kipofu alimtii Yesu bila kuona. Lakini matokeo yake, alipata kuona papohapo; ambapo baadaye, hatimaye, alipokea uponyaji halisi wa kiroho.

Enock Maregesi
Save QuoteView Quote